Monday 25 November 2019

Magari 5 Yasiotumia Mafuta Mengi nchini Tanzania

Zaidi ya kuwa bugudha, foleni inaongeza matumizi ya mafuta, hasa kwenye miji ya watu wengi kama Arusha, Mwanza na Dar. Iwapo, kuwa tabia za kubana matumizi ya mafuta kama kudumisha gari lako, kuzima AC na kuendesha kwa spidi ya kawaida yatasaidia, bora uwe na gari isiyotumia mafuta mengi. Uzuri wa magari yasiotumia mafuta mengi ni kwamba si lazima yawe ghali. Na tumeziorodhesha hapa.

Image result for ist new model
Ist 
 1. Toyota IST
 IST ni gari ambayo wanunuzi wake ndio mara yao ya kwanza kuwa na gari au watu wenye bajeti ya kawaida wanaotaka gari la kila siku ambayo ni rahisi kuidumisha. Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 12m.

 2. Toyota Vitz
 Vitz inafanana na IST kwenye utendaji ila ni ndogo zaidi na nafuu zaidi. Ila, injini yake ina nguvu yakutosha. Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 9m.

 3. Toyota Passo
 Kwa swala la ubunifu, Passo ni kubwa zaidi ya Vitz ila ikijia kwenye maswala ya utendaji, yanatofautiana kidogo sana. Watu watano wanatosha kwenye gari hii pamoja na mizigo na pia, gari linaweza kutembea 100km kwa lita 7. Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 8.5m.

 4. Nissan March
 Ingawa inaonekana ndogo, ndani kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa sababu ya jinsi matairi yalipowekwa pamoja na uwezo wa viti vya nyuma kuvunjwa. Pia, udogo wake inaiwezesha kupenya barabarani. Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 4m – TZS 6m.

 5. Honda Fit
 Ubunifu wa Honda Fir ndio kinachoiwezesha kuwa na matumizi mazuri ya mafuta. Badala ya kuifanya iwe kubwa zaidi, na hivyo kuongeza uzito wake, Honda waliamua kwamba wataongeza nafasi kwa kuweka tenki la mafuta chini ya viti vya mbele na kupandisha viti vya nyuma. Hii imewezesha gara hii kutembea 100km kwa 7.1L. Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 14m. Faida haziishi Kuwa na gari yenye matumizi mazuri ya mafuta itakupunguzia gharama ya uendeshaji sana! Sasa kwa kuwa una chaguo za magari yasiotumia mafuta mengi

 Share and give your comment

About the Author

Mussa Msemakweli is a technology entrepreneur, Book writer and digital marketing expert. He is currently C E O at the Africa shared . His work has been featured in a number of publications, including the Maisha halisi Magazine and on Culture trip. If you have a good time follow me on facebook and instagram or leave a comment, Thanks.
Follow Me on Facebook Facebook maishahalisi_tanzania FOLLOW'>Instagram


Mussa Msemakweli

No comments:

Post a Comment