Saturday, 22 August 2015

Mbegu za maboga huongeza nguvu za kiume ,soma faida 7 kiafya za kutumia mbegu za maboga




Mbegu  za  maboga  zina  faida  nyingi  sana  kwa  afya  ya mwanadamu.   Mbegu  za  maboga   zimethibitika  kuwa  na kiwango  kikubwa  cha  virutubisho  vya  aina  mbalimbali kuanzia  magnesium, manganese, shaba, protini, zinki nakadhalika.  Zifuatazo  ni  baadhi  ya  faida  za  matumizi ya  mbegu  za  maboga.
  1. KuongezaMaziwa  Kwa  Wanawake  Wanao  Nyonyesha : Kwa  wanawake  wanao  nyonyesha  matumizi  ya  mbegu za  maboga  huwasaidia  kuongeza    kiwango  cha  maziwa yenye  afya  kwa  watoto  wanao  nyonya.
  1. Mbeguza  maboga  zina  zina  kiwango  kikubwa  cha madini   ya  magnesium  ambacho  mwanadamu  anatakiwa kukitumia  kila  siku.
  1. Mbegu za  maboga  zina  kiwango  kikubwa  cha  madini ya  zinc  ambayo  yana  faida   mbalimbali  katika  mwili  wa mwanadamu  kama  vile  kuimarisha  kinga  ya  mwili, kuimarisha  uwezo  wa  kuonja na  kunusa, ukuaji  wa  seli mbalimbali  za  mwilini, kuimarisha  afya  ya  macho  na ngozi, kulinda  na  kuimarisha  insulin pamoja  na kuongeza  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa wanaume.
  1. Mbeguza  maboga  ni  miongoni  mwa  vyanzo  bora kabisa  vya  mafuta  na  acid zitokanazo  na  mimea  ambazo  zina  faida  kubwa  sana  kwa  afya  ya  mwili  wa mwanadamu.
  1. Mbeguza maboga  zinasaidia  katika  kulinda  na   kuimarisha  ufanisi  wa  tezi  kwa  wanaume
 Mbegu  za  maboga  zina  faida  kubwa  sana  kwa wagonjwa  wa  kisukari  kwani  zinasaidia  katika  kulinda, kuboresha,  kuimarisha   na  kurutubisha  insulin
  1. Mbeguza  maboga  zina  imarisha  na  kulinda  afya  ya moyo  na  ini
  2. Mbeguza  maboga  zinasaidia  katika  kuboresha  usingizi. Kama  una  matatizo  ya  usingizi  unashauriwa  kutafuna mbegu  za  maboga  pamoja  na  tunda  kidogo. Hii itakusaidia  katika  kupata  usingizi  mzuri.
Anza  kujenga  tabia  ya  kuwa  unatumia  mbegu  za maboga  kwa  faida  mbalimbali   kwa  afya  ya  mwili  wako kama  ilivyo  onyeshwa  hapo  juu.   Kwa  makala mbalimbali  za  afya  na  tiba a silia, endelea  kutembelea

About the Author

Mussa Msemakweli is a technology entrepreneur, Book writer and digital marketing expert. He is currently C E O at the Africa shared . His work has been featured in a number of publications, including the Maisha halisi Magazine and on Culture trip. If you have a good time follow me on facebook and instagram or leave a comment, Thanks.
Follow Me on Facebook Facebook maishahalisi_tanzania FOLLOW'>Instagram


Mussa Msemakweli

No comments:

Post a Comment